Simba Vs Yanga Kwa Mkapa, Azam Vs Coastal Zanzibar Ngao Ya Jamii
Shirikisho la mpira Tanzania kupitia Bodi ya ligi limetangaza ratiba rasmi ya Ngao ya Jamii 2024 ambapo inatarajiwa kuanza Agosti 08, 2024 katika viwanja vya Tanzania Bara na visiwani. Mchezo wa kwanza ni kati ya Azam FC dhidi ya Coastal Union utakaochezwa katika dimba la Uwanja wa Amaan, Zanzibar Agosti 8, 2024 majira ya saa 10 jioni. Mchezo wa pili wa Dabi ya Kariakoo utachezwa Agosti 8, 2024 katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 1 Jioni. Fainali ya mashindano hayo yanatarajiwa kuchezwa Agosti 11, 2024 katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 1 jioni. Unaweza ukashea hii popote pale na wengine wafahamu!!